Ripoti ya ABNA inaeleza kwamba; Licha ya hatua hiyo ya Mfalme Abdullah upinzani nchini humo ulishiriki katika maandamano makubwa siku ya Ijumaa kushinikiza mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi nchini humo, pamoja na kutaka mamlaka za Mfalme huyo kupunguzwa.
Maandamano hayo yalohudhuriwa zaidi ya waandamanaji Laki tano huku kundi lingine ambalo lilikuwa limepanga maandamano ya kumuunga mkono Mfalme Abdullah kwa kulivunja bunge likisitisha maandamano yake.
Kiongozi huyo wa Jordan kwa muda mrefu amekuwa akitaka uchaguzi mpya kufanyika nchini humo mapema mwakani, uchaguzi ambao upinzani unasema hautashiriki bila la kuwepo kwa mabadilko ya kisiasa na kiuchumi nchini humo.
Upinzani katika hatua nyingine unataka sheria ya uchaguzi kubadilishwa, baada ya sheria iliyokoo kwa sasa kutozingatiwa baada ya Mfalme kulivunja tena bunge mwaka 2010.
Maandamano nchini Jordan yamekuwa yakifanya tangu mwezi Januari kushinikiza mabadiliko.